Leo ilikua ni siku nyingine ambayo inasubiriwa kwa hamu na upande wa Mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ambapo alipeleka maombi ya kupata dhamana Mahakama kuu hivyo leo ndio jibu lilikua linatolewa.
Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo umetoka ambapo Mahakama hiyo imetupilia mbali maombi ya dhamana ya Manji na kukubaliana na pingamizi la upande wa Serikali ambapo maombi hayo yametupiliwa mbali na Jaji Isaya baada ya kusema anakubaliana na hoja za upande wa serikali.
0 comments:
POST A COMMENT