NEEMA YAZIDI KUVISHUKIA VILABU VYA TANZANIA SAFARI HII NI ZAMU YA NDANDA | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Tuesday, August 15, 2017

NEEMA YAZIDI KUVISHUKIA VILABU VYA TANZANIA SAFARI HII NI ZAMU YA NDANDA


Ndanda Sports Club ya Mtwara imesaini mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na kampuni ya Motisun Group ambao ni watengenezaji wa bidhaa zenye chapa ya Kiboko.
Kwa mujibu wa Motisun Group, thamani ya mkataba huo inakaribia ile ya mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara.
“Tumesaini mkataba wenye thamani kubwa lakini hatuta weka wazi ni kiasi gani cha pesa. Udhamini wetu kwa Ndanda utakuwa ukikaribiana na wa mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara,” Erhard Mlyansi afisa masoko Motisun Group.
“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja lakini kutokana na mahusiano yaliyopo tutakuwa tukipokea maombi kutoka Ndanda juu ya mahitaji yao na kufanyia kazi yale tutakayoona tunayaweza.”
Mshauri wa Ndanda katika masuala ya biashara Bw. Peter Simon amesema, watahakikisha Motisun wanapata nafasi ya kujitangaza kupitia Ndanda SC.
“Sisi Ndanda tutawapa Motisun Group nafasi ya kujitangaza kupitia mabango ambayo yatawekwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani.”
“Ndanda itacheza mechi 15 kwenye uwanja wake wa nyumbani, Motisun watapata fursa ya kuonekana kwenye mabango mawili katika kila mechi ambazo tutacheza Mtwara.”

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT