MKWASA AMZUNGUMZIA TSHISHIMBI NA KUKILI WAMEPOTEZA MAWASILIANO NAE | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Saturday, August 12, 2017

MKWASA AMZUNGUMZIA TSHISHIMBI NA KUKILI WAMEPOTEZA MAWASILIANO NAE




WAKATI waandishi wakijaa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, kumsubiri kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa, amesema mawasiliano na staa huyo yamepotea.


Awali ilitangazwa kuwa mchezaji huyo raia wa Congo DR angetua nchini saa nane za mchana huu, lakini hadi sasa hajatua na katibu huyo amesema mwanzo walikuwa na mawasiliano naye lakini ghafla yamepotea na hawajui atatua saa ngapi.

“Sijui atatua saa ngapi, tumepoteza mawasiliano naye tukimtafuta hatumpati, hivyo kama atakuja baadaye basi tutawataarifu,” alisema Mkwasa.

Tshishimbi raia wa DR Congo, tayari alimalizana na Yanga katika suala la mazungumzo na Yanga wakaingia mazungumzo na klabu yake ya Mbabane Swallows.

Kilichokuwa kinasubiriwa ni Mcongo huyo kurejea kwa ajili ya kusaini mkataba na Yanga ili achukue nafasi ya Justice Zulu, kiungo mkabaji kutoka Zambia aliyeshindwa kuonyesha cheche za "ukataji umeme".

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT