OMOG AHESABIWA SIKU ZA KUBAKI AU KUONDOKA SIMBA NDANI YA MUDA HUU | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Friday, August 11, 2017

OMOG AHESABIWA SIKU ZA KUBAKI AU KUONDOKA SIMBA NDANI YA MUDA HUU






Na Saleh Ally
MAKOCHA wenye presha kubwa msimu huu kama utazungumzia soka la Tanzania basi ni Hans van der Pluijm wa Singida United na Joseph Omog wa Simba.

Leo ningependa nimzungumzie Omog raia wa Cameroon ambaye msimu uliopita, unaweza kumchagua kuwa kocha bora wa msimu kwa kuwa amefanya mambo mawili makubwa.

Kwanza, ameiwezesha Simba kumaliza msimu ikiwa ya pili, nafasi ambayo ilikuwa ikihaha kuipata kwa misimu minne iliyopita. Kama haitoshi, Omog ameiwezesha Simba kumaliza na pointi 68 sawa na mabingwa Yanga kukiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga haikuwahi kumaliza na tofauti chini ya pointi tano dhidi ya Yanga kwa zaidi ya misimu minne. Hivyo hata kama ataonekana si kocha mwenye mbwembwe nyingi lakini kazi yake aliifanya kwa ufasaha mkubwa na hakika ni mtu anayestahili pongezi kwa kuwa amerejea Tanzania kwa mara ya pili baada ya kuipa ubingwa Azam FC na kuonyesha ni kocha anayeweza tena.

Hiyo ni katika Ligi Kuu Bara, lakini angalia ameirudisha uhai wa Simba kwa kuiwezesha kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho. Maana yake, Simba inarejea katika michuano ya kimataifa kwa mara nyingine baada ya zaidi ya misimu minne, jambo ambalo lilikuwa kero kubwa kwa Wanasimba. Ndiyo maana nasema, ni kocha anayestahili pongezi zake badala ya lawama pekee.

Lakini bado unaona, huenda msimu huu ukawa wenye furaha kubwa kwa Omog raia wa Cameroon lakini pia unaweza ukawa wa wenye machungu ya kupitiliza hali inayoweza kuzaliwa na presha.

Nasema presha kwa kuwa mashabiki wa Simba wamejenga imani kubwa, matumaini makubwa na matarajio ya juu kuhusiana na kikosi chao. Hii inakwenda pia kwa viongozi ambao wameamua kufanya kila kinachotakiwa kwa kusaini kikosi imara, chenye wachezaji wenye uzoefu na maandalizi ya kutosha.

Walichokifanya wao ni kama vile wamemaliza kazi iliyotakiwa na baada ya hapo, wameangusha kila kitu kwa Omog na sasa wanachosubiri wao ni matokeo ambayo yataendana na mafanikio.
Ninaamini kama niko sahihi, siku 29 zitaamua hatma ya Omog kama atakuwa ni mtu mwenye amani au raha ndani ya Msimbazi au safari itamkuta kwa kufungashiwa virago vyake.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT