Leo August 4, 2017 Mfanyabiashara Yusuf Manji anayekabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu ana kesi nyingine Mahakama Kuu.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, kueleza kesi imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, na upelelezi wa kesi haujakamilika lakini Mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Manji ameshindwa kwa sababu ana kesi nyingine Mahakama Kuu.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi August 9, 2017 kwa ajili ya kutajwa ingawa washtakiwa wenzake ambao ni Deogratias Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwele wamefika Mahakamani.
0 comments:
POST A COMMENT