NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke anawatangazia wananchi/ watanzania wote wenye sifa zinazotakiwa kuomba kujaza nafasi mbalimbali za kazi kama zilivyoainishwa hapo chini
KATIBU MAHSUSI DALAJA LA III NAFASI 2
SIFA/ELIMU
- elimu ya kidato cha IV
- waliohitimu mafunzo ya uhazili na kufahulu mitihani ya hatua ya III
- walio fahulu somo la hati mkato ya kiswahili na kingereza maneno 80 kwa dadkika
- waliopata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinacho tambulika na serikali na kupata cheti katika programme ya windows/ microsoft excel, office, internet/email na publisher
KAZI NA MAJUKUMU
- kuchapa barua/taarifa na nyaraka za kawaida
- kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
- kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake kajalada, nyaraka, au kitu chochte kinachohitajika katika shughuliza lazki hapo ofisin
- kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumwarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi wake
- kusaidia kutunza taarifa, kumbu kumbu, za matukio , miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mku wake na taaatibu za kazi zingine zilizopnangwa kutekelezwa katika ofisi anazomfanyia kazi na kumwarifi mkuu wake kwa wakati unao hitajika
NGAZI YA MSHAHARA TGS.B
MSAIDIZI WA KUMBU KUMBU DARAJA LA II NAFASI 3
SIFA ZA KUAJIRIWA
- mwombaji awe na cheti cha kidato cha nne/sita wenye cheti cha utunzaji wa kumbu kumbu wa fani ya masijala
KAZI ZA KUFANYA
- kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayo hitajika na wasomaji
- kuthibiti upokeaji, uandikishwaji wa kumbukumbu /nyaraka
-kuchambua, kuorodhesha, na kupanga kumbukubmu/nyaraka katika makundi na somo
- kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki katika masijala
-kuweka kumbukubmu/barua nk katika mafaili
- kushughulikia maombi ya kumbukumbu /nyaraka kutoka taasisi za serikali
NGAZI YA MSHAHARA TGS.B
DEREVA DALAJA LA II NAFASI 1
SIFA/ELIMU/UJUZI
- Elimu ya kidato cha IV
- mwenye leseni ya daraja C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali
- menye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II
kazi na majukumu
- Kuendesha magari ya abiria na malori
- kuhakikisha vyombo vyotake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unao hitaji matengenezo
- kufanya matengenezo madogomadogo katika gari
- kutunza daftari la safari log0book kwa safari zote
NGAZI YA MSHAHARA TGOS I
UMRI
waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usipungua miaka 18 na usizid miaka 45
MAELEZO YA JUMLA
maombi yote yawasilishwe yakiwa yameambatanishwa na CV pamoja na nakala za vyeti vy kuhititmu elimu na mafunzo vyeti vitakavyoonyesha kiwango cha kufaulu na sio leaving certificate
MUHIMU
muombaji anatakiwa vyeti vyake halisi na halali kwani uhakiki utafanyika katika vyuo ulivyopitia pamoja na baraza la mitihan. danganyifu wowote ukibainika hatua za kisheria zitachuliwa
MAOMBI YATUMWE KWA
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,
S.L.P 46343
DAR ES SALAAM
mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Ijumaa tarehe 25/08/2017 saa 9 lasiri
0 comments:
POST A COMMENT