Imeelezwa ndani ya saa 48 kwa asilimia 80 inaonekana Neymar atakuwa mchezaji wa PSG ya Ufaransa.
Taarifa zinaeleza, Barcelona iko katika nafasi ya kumuachia Neymar ili kuepuka kumlipa baba mzazi wa mchezaji huyo, Neymar Sernior kitita cha euro milioni 26.
Katika mkataba alioingia na Barcelona akitokea Santos ya kwao Brazil, unaeleza kuwa kama akiongeza mkataba mpya na Barcelona, basi baba yake huyo ambaye ni meneja wake anapaswa kulipa kitita cha euro milioni 26.
Imeelezwa hali hiyo inaikera Barcelona na inataka kuiepuka kwa hali na mali na ndiyo inayoweka uhakika kwamba itamuachia ajiunge na Barcelona ili isilipe fedha hizo.
Pamoja na hivyo, imeleezwa mastaa wengi wa Barcelona wanaonekana kuchoshwa na mambo hayo ya Neymar anaondoka, anabaki mara kapigana hivyo wangependa “Aende zake”.
0 comments:
POST A COMMENT