Baada ya headlines za muda mrefu katika mitandao ya kijamii kuhusiana na ishu ya golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 aliyeshiriki katika michuano ya AFCON U-17 Gabonmwaka huu Ramadhani Kabwili kusajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka mitano.
AyoTV imempata afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas azungumzie kuhusiana na kinachoendelea, kwa kanuni za usajili inasemwa kuwa mchezaji chini ya umri wa miaka 18 hawezi kusaini mkataba wa miaka mitano mwisho ni miaka mitatu, vipi kwa Kabwili ambaye hajafikia umri huo?
“Kwanza niwaondoe hofu watanzania ukiondoa suala la vyetu ambapo zimewekwa tarehe kama mbili katika mitandao, timu haizuiwi kumsajili lakini matumizi ya mchezaji yatasubiri tarehe husika ili aweze kutumika maana wana nafasi ya kumkuza baada ya miezi mitatu anatimiza miaka 18” >>> Alfred Luca
s
s
0 comments:
POST A COMMENT