Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi tayari ameanza mazoezi na wenzake na ameonekana si mgeni katika kikosi hicho.
Simba imeweka kambi jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, kujiandaa na msimu mpya wa 2017-18 na kikosi chake kitaanza kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza wakivaa Rayon ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa siku ya tamasha la Simba Day.
Jambo la pili ambalo ameonyesha Okwi baada ya kuanza mazoezi, anaonekana ni mtu aliyekuwa akijifua au alifanya mazoezi kutokana na kuwa katika kikosi cha timu ya taifa.
Kwani anaonekana kuwa fiti na mwepesi licha ya kwamba mazoezi waliyofanya ni yale ya kupasha misuli.
“Okwi anaonekana yuko vizuri tu na ameonekana ni mwenye furaha baada ya kuungana nasi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
Kitu kingine kizuri ni Okwi kupokelewa na wachezaji wa Simba wa zamani wakiwemo wale wapya ambao pia anawajua kwa kuwa aliwahi kukutana nao akiwa Simba na wao wakiwa na timu zao kam Azam FC, Mtibwa Sugar na kadhalika.
0 comments:
POST A COMMENT