Jerry Tegete ameonyesha kufurahia kusajiliwa Majimaji ya Songea.
Tegete amesema anaamini Majimaji inakuwa maisha yake mapya ya soka na anatamani kufanya vema.
“Maisha ya soka haujui utaenda wapi, lakini ninataka kurudisha kiwango changu na kufanya vizuri zaidi nikiwa na Majimaji,” alisema.
Tegete ameondoka Mwadui FC na kujiunga na Majimaji ambaye msimu uliopita ilifanya kazi ya ziada kujikomboa isiteremke daraja.
Tegete alikuwa kinara katika ufungaji wakati akiichezea Yanga.
0 comments:
POST A COMMENT