SIMBA wameamua bwana, hawataki mchezo msimu huu kwenye ujenzi wa kikosi chao na leo mkoba raia wa Tanzania Paul Bukaba anayekipiga na Atletico Olympic ya Burundi amemalizana na Wekundu hao kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutua Sauzi usiku wa jana.
Tetesi za kutua kwa nyota huyo ambaye hakuwahi kutamba sana hapa nchini zilianza kuzagaa usiku wa jana baada ya kuonekana katika uwanja wa ndege wa Kigali akisubiri ndege kwa ajili ya safari ya Sauzi.
Bukaba aliwahi kucheza nchini DR Congo katika klabu ya OC Muungano ambapo kwa Tanzania aliichezea Toto Africa kwa kipindi kifupi kabla hajatimkia zake Burundi.
Kusajiliwa kwa beki huyo kunaongeza tetesi za kuuzwa kwa kisiki Juuko Murshid katika moja ya klabu kubwa huko Sauzi.
0 comments:
POST A COMMENT