Hii leo Manchester United wamekamilisha usajili wao wa tatu baada ya kumnunua kiungo Nemanja Matic kutoka Chelsea usajili ambao umekuwa ukitajwa kwa muda mrefu sana.
Mourinho amekuwa akimhitaji Matic kwa muda sasa na kiasi cha £39.7m kimetosha kumsaini Matic na kumpa mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja hapo baadaye.
Usajili wa Matic aliyepewa jezi namba 31 una faida kubwa kwa Paul Pogba ambaye amekuwa na msimu usio mzuri sana toka ajiunge na Manchester United tofauti na wakati akikipiga Juventus.
Pogba bado ni bora lakini kuna vitu anakosa United ambavyo alikuwa akivipata alipokuwa Juventus na hii ndio imempa mzigo mkubwa sana ndani ya United kiasi cha kupelekea makali yake kutoonekana.
Matic anakuja United na Mourinho anaweza kujaribu kuchezesha 4-3-3 au 4-2-31 na mifumo yote hii inamfanya Pogba kuwa mbele ya viungo wawili ambao wanaweza kuwa Hererra na Matic,Fellaini na Matic au Carrick na Matic.
Matic wakati akiwa Chelsea uimara wake na ukabaji wake vilimfanya Cesc Fabregas ambaye alianza kuonekana kupotea kama ilivyo kwa Pogba lakini kiwango cha Matic kilimfanya Fabregas kupiga assists 18 msimu wa 2014/2015 na Chelsea wakabeba ndoo.
Lakini ujio wa Matic unaweza kuwa habari mbaya kwa Marouane Fellaini ambaye tayari kocha wake Jose Mourinho ameshasema ni rahisi kwake kuondoka kuliko kumuuza Fellaini kwenda klabu yoyote.
Msimu uliopita Fellaini amesota sana benchi na kiwango cha Ander Herrera kilimfanya kuzima kabisaa na mara nyingi akatumika kama mchezaji wa ziada akiingia kipindi cha pili cha mchezo.
Huu ni usajili wa 3 wa United msimu huu baada ya Victor Lindelof na Lukaku, nani atafuata kusajiliwa baada ya Nemanja Matic?ni Ivan Perisic kutoka Inter Millan au United watakamilisha usajili wa Serge Aurier toka PSG?
0 comments:
POST A COMMENT