George Weah kuwania urais Liberia Oktoba | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Monday, July 31, 2017

George Weah kuwania urais Liberia Oktoba


George Weah aliwania urais mara ya kwanza 2005Haki miliki ya pichaAFP
Image captionGeorge Weah aliwania urais mara ya kwanza 2005
Baada ya kuongoza kwa mwongo mmoja kama rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, atastaafu baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwezi Oktoba.
Orodha kamili ya wanaowania kumrithi mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel sasa imejulikana, shirika la habari la AFP limeripoti.
Kuna jumla ya wagombea 20.
Miongoni mwa wagombea hao ni nyota wa zamani wa soka George Weah, ambaye alishindwa na Johnson Sirleaf uchaguzi wa mwaka 2005.
Jewel Howard-Taylor, 54, mke wa zamani wa Charles Taylor atakuwa mgombea mwenza wa Bw Weah.
Mbabe wa kivita wa zamani Prince Johnson pia anataka kuongoza taifa hilo.
Shirika la habari la AFP linasema kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani.
Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 10 Oktoba.


google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT