SINGANO APAGAWISHA WAARABU, KONA ZOTE GUMZO | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Monday, July 31, 2017

SINGANO APAGAWISHA WAARABU, KONA ZOTE GUMZO



Kiungo kinda wa pembeni wa Difaa Al Jadid ya Morocco, Ramadhani Singano Messi ameonyesha kuwa kivutio baada ya mechi yake ya kwanza ya kirafiki akiitumikia klabu hiyo.

Mechi hiyo Difaa Al Jadid ilipoteza kwa mabao 2-1 huku Mtanzania mwingine, Simon Msuva akifunga bao la kufutia machozi.

Lakini wachambuzi kadhaa wa soka wameonyesha kuvutiwa na Singano ambayo alicheza kwa kujiamini na kutoa msaada mkubwa.

Katika uchambuzi wa runinga moja ya michezo, zaidi wameeleza alivyokuwa mwepesi kutoa pasi na kuchukua nafasi na mwisho kujumuisha kwamba, “Watanzania hao wakizoea Ligi ya Morocco, watakuwa hatari zaidi”.


Singano amejiunga na timu hiyo akitokea Azam FC baada ya mkataba wake kumalizika.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT