Usain Bolt amepoteza shindano lake la mwisho la mita 100 baada ya kusgindwa na Mmarekani Justin Gatlin katika mashindano ya dunia ya IAAF jijini London, Uingereza.
Katika mashindano hayo yaliyomalizika hive punde, Bolt ameambulia nafasi ya tatu na Gatlin aliyewahi kuingia kwenye kasha ya kutumia dawa za kuongeza nguvu akiibuka na ushindi.
Bingwa huyo mara nane wa mitt 100 na 200, alionekana mzito mwanzoni na mwisho akashindwa kuchanganya kama ilivyozoeleka.
Mwisho Gatlin aliyekuwa nyuma akaongeza kasi na kumpita na Mmarekani mwingine, Christian Coleman akampita na kushika nafasi ya pili.
Hata hivyo, mashabiki waliendelea kumuaga Bolt kwa shangwe kubwa katika shindano lake hilo la mwisho.
0 comments:
POST A COMMENT