Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii watakaocheza dhidi ya Simba, wachezaji watatu wa kikosi hicho hawapo kambini kutokana na sababu za majeraha.
Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao ambapo amesema kwa mujibu wa daktari wa timu watatu hao hawatakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi ya Ngao ya Jamii.
“Beno Kakolanya, Geoffrey Mwashiuya na Obrey Chirwa hawapo Pemba kwenye kambi kutokana na majeraha ambayo wanaendelea kujiuguza,” Dismas Ten.
“Daktari wa timu Dkt. Bavu amethibitisha wataendelea kukaa nje kwa muda, ni wazi kwamba wachezaji hawa hawatakuwa sehemu ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba August 23, 2017.”
“Timu inatarajia kurejea Dar siku moja kabla ya mchezo (August 22).”
Mechi ya Ngao ya Jamii itakuwa imezindua rasmi ligi kuu Tanzania bara ambapo August 26, 2017 mechi za ligi zitaanza kuchezwa kwenye viwanja tofauti.
0 comments:
POST A COMMENT