Yanga imeonja utamu wa kipigo kwa msimu wa 201-18 baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki.
Yanga imepoteza dhidi ya Ruvu Shooting, ukiwa ni mchezo wa mwishomwisho kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.
Kabla ya mechi hiyo, msemaji wa Shooting, Masau Bwire alitamba "watawanyoa" Yanga na kuwaonyesha soka si majina badala yake ni uhakika wa kucheza na kupanga mipango ya kummaliza adui.
Bao hilo la Ruvu Shooting lilikuwa ni “zawadi” kutoka kwa beki Abdullah Shaibu.
Shaibu maarufu kama Ninja, alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira langoni mwake.
Juhudi za washambulizi wa Yanga kutaka kurudisha bao hilo licha ya kulisakama lango la Shooting kama nyuki, hazikuzaa matunda.
Kwa kuwa kulikuwa na ucheleshwaji wa muda, mwamuzi aliongeza muda hadi kufikia dakika 98, lakini washambulizi wa Yanga hawakuweza kuipenya ngome ya wanajeshi hao iliyokuwa imara zaidi na zaidi.
0 comments:
POST A COMMENT