Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kuhusu hali ya Mohamed Hussein ambaye aliumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Gulioni.
“Tshabalala atakuwa vizuri hana tabu yoyote, tnashukuru sana mapokezi ya mashabiki wetu wote wametupokea vizuri naomba waje kwa wingi siku ya Jumatano kwenye mechi ya Ngao ya Jamii,” Jackson Mayanja.
“Waje kwa sababu hii ni timu yao, Simba Nguvu Moja lazima waje kwa wingi kwa sababu hiyo ni mechi ya derby.”
Tshabalala alicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Gulioni tangu alipoumia kwenye mechi ya fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup May 27, 2017 Simba ilipocheza dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Simba wapo Zanzibar (Unguja) tangu Jumatatu August 14, 2017 wamecheza mechi mbili za kirafiki hadi sasa dhidi ya Mlandege na kutoka suluhu hku mechi yao ya pili wakishinda 5-0 dhidi ya Gulioni. Timu inatarajia kurejea Dar Jumanne (kesho) August 22 kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Yanga.
0 comments:
POST A COMMENT