Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema wamewaweka chini wachezaji wao na kuwaeleza kuwa makini na kuongeza juhudi la sivyo, watapoteza mechi dhidi ya Yanga.
Simba itaivaa Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa wikiendi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hans Poppe amesema, suala la wachezaji kujiamini kupita kiasi limekuwa ni tatizo katika mechi zinazowakutanisha watani.
"Unajua kawaida wale wanaoonekana ni underdog (wasindikizaji), uliona mechi yetu ya mwisho na Yanga. Tulionekana hatuna kitu na wao wako vizuri, mwisho tukawapiga na wale waliokuwa wakitabiri hadi kuweka matokeo wakabaki kimya," alisema.
"Sasa na sisi kama hiyo tutaipa nafasi, mwisho yatakuwa kama hayo yaliyowakuta Yanga. Hii imekuwa ikitokea sana na kama wewe una timu nzuri, basi unachotakiwa ni kupambana na kufunga.
"Tumewaambia wachezaji, mpira hauwezi kuingia langoni wenyewe. Badala yake kila mmoja anatakiwa kujituma kwa nafasi yake na kufanya vizuri.
"Ukiwa mchezaji bora, msaada wako unatakiwa kuonekana na kusaidia matokeo mazuri na hata kama ni kufunga. Basi wafunge mabao kweli, si bao moja moja tu."
Pamoja na Hans Poppe kusema hivyo, hata mashabiki wa Simba nao wamewaonyesha wachezaji wao kwa kuonyesha kujiamini kupindukia kwa kuwa inaweza kuchangia kupoteza mechi dhidi ya Yanga.
0 comments:
POST A COMMENT