Usiku wa August 16 2017 mchezo wa marudiano wa Super Copa kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona ulichezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, kipindi ambacho FC Barcelona waliingia uwanjani wakiwa nyuma kwa magoli 3-1 waliyofungwa Nou Camp katika mchezo wa kwanza.
FC Barcelona ambao waliingia uwanjani kutafuta magoli ya kusawazisha na hatimae kupata Ubingwa huo, wamejikuta wakiambulia kipigo kingine kwa kufungwa magoli 2-0, magoli ya Real Madrid yakifungwa na Marco Asensio dakika ya 4 na Karim Benzemadakika ya 38.
Mara ya mwisho Real Madrid na FC Barcelona kukutana katika mchezo wa Super Cop ilikuwa August 30 2012 katika uwanja wa Santiago Bernabeu na Real Madrid kushinda kwa magoli 2-1 licha ya game ya kwanza iliyochezwa Nou Camp kupoteza kwa magoli 3-2 ila aggregate ikambeba kwa kufunga magoli mengi ugenini.
0 comments:
POST A COMMENT