Athumani Iddi ‘Chuji’ amerejea Ligi Kuu Bara baada ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara.
Chuji amerejea kwa kusaini mwaka mmoja kuichezea Ndanda ambayo msimu uliopita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, alipotea baada ya kuachwa na Yanga misimu mitano iliyopita.
Juhudi zake za kurejea Ligi Kuu Bara zilionyesha kutokuwa na mafanikio hata alipojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo licha ya kukaa misimu miwili, hakupata nafasi ya kucheza.
Baada ya hapo, Chuji aliamua kujiweka kando mwa ligi hiyo na hivi karibuni aliibuka na kufanya vizuri katika michuano ya Ndondo FC.
0 comments:
POST A COMMENT