ALICHOAMBIWA MSUVA NA KOCHA WAKE KABLA YA KUINGIA UWANJANI NA KUFUNGA GOLI MECHI YAKE YA KWANZA | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Monday, July 31, 2017

ALICHOAMBIWA MSUVA NA KOCHA WAKE KABLA YA KUINGIA UWANJANI NA KUFUNGA GOLI MECHI YAKE YA KWANZA

Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Simon Msuva aliyekuwa anaichezea Yanga, Jumapili ya July 30 ikiwa ni siku nne zimepita toka asaini mkataba na timu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ambapo ni mafanikio kutoka kucheza Tanzania nchi iliyopo nafasi ya 114 katika viwango vya FIFA anakwenda kucheza nchi iliyopo nafasi ya 60.
July 30 amepata nafasi ya kuichezea timu yake ya Jadid mchezo wa kwanza wa kirafiki na kufunga goli wakipoteza kwa magoli 2-1, kocha wa Jadid alimpanga Simon Msuva dakika 45 za pili licha ya kupoteza mchezo huo Msuvandio alifunga goli la kufutia machozi kwa upande wa Difaa El Jadid.
millardayo.com imempata Simon Msuva katika EXCLUSIVE INTERVIEW baada ya mechi kutokea Morocco, vipi hali ilikuwaje katika mchezo wa jana
“Nashukuru Mungu nimecheza game yangu ya kwanza ya kirafiki na timu ya huku ipo daraja la kwanza, dakika 45 za pili nikaingia lakini mwalimu aliniuliza maswali na kuniambia ananichezesha namba 10 kwa sababu mimi nafunga haoni haja ya kunichezesha winga.” – Msuva.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT