Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia ambayo imelenga kushughulikia masuala uwezeshwaji wa wanawake na huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini kwa wakati mwafaka
Wakati wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Makamu wa Rais alisema kuwa Merck Foundation inakaribishwa na serikali inatarajia kushirikiana na taasisi hiyo inayoheshimika na iliyo makani katika kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya na sayansi.
Tunatambua mchango unaotolewa na Merck Foundation katika kujengea uwezo huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake nchini Tanzania, hususani katika kampeni zinazolenga kuuongezea umma uelewa kuhusu ugumba.
Makamu wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini Tanzania na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya katika kuheshimu na kumtambua wanawake kama sehemu ya wanajamii wanaozalisha wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.”
Merck Foundation hali kadhalika imejikita katika ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania katika kuijengea uwezo katika huduma za afya na kuboresha kufikiwa kwa ubunifu na masusluhisho yaliyo katika uwiano kote nchini ikiwa ni sehemu ya program za uwajibikaji kwa jamii barani Afrika.
“Merck Foundation itatilia mkazo katika uwezeshwaji wa wanawake walio na tatizo la ugumba kupitia upatikanaji wa taarifa, uelewa, afya, kubadili mitazamo na kuwewawezesha kiuchumi kote nchini kupitia kampeni ya Merck ya Zaiidi ya mama,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck, Dk. Rasha Kelej.
Kampeni hiyo ambayo inatoa msukumu kwa vyombo vya habari na wadau wengine kuchpisha na kuwasilisha mada kwa njia ya mtandao, video na vipindi vya redio kuhusu masuala yanayohusu ugumba ilizinduliwa nchini Tanzania Juni mwaka huu. Washindi katika kampeni hiyo wanatarajiwa kuondoka na zawadi ya fedha kuanzia dola 1000 hadi dola 5000.
“Tatizo la ugumba barani Afrika ni kubwa, inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya kila watu wane walio na umri wa kuzaa anasumbuliwa na tatizo la ugumba, na takribani asilimia 85 wale walio na tatizo la ugumba linatokana na ukosefu wa tiba kwa ugonjwa ambao unaweza kutibika, hivyo kuongeza uelewa kuhusu kuzuia hali hiyo kupiti vyombo vya habari vya ndani na mitandao ya jamii ni hatua muhimu.”, alisema Dk. Rasha Kelej’’
Aliongeza, “Kujenga uelewa kuhusu ugumba kwa wanaume kwani ugumba una athari sawa kwa wanaume na wanawake, lakini wamekuwa ndio wanaolaumiwa peke yao, wanatengwa na kudhalilishwa ndani ya jamii zao. Kampeni itashughulikia mada hizi na kutoa msukumo kwa wanaume kujadili kwa uwazi tatizo lao la ugumba na kushirikiana katika safari ya kutambua ugumba na matibabu ya wake zao.”
Kwa upande mwingine Merck foundation itajikita zaidi katika kugharamia mafunzo kwa wataalamu wa afya kwenye maeneo ya saratani kwa watoto (paediatric oncology) katika programu za udhamini nchini India, Ulaya na katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa madaktari wa Tanzania ili kuboresha upatikanaji wa huduma zote zinahusu saratani.
Hivi karibuni Merck ilizindua Tuzo ya Kuvitambua Vyombo vya Habari kupitia kampeni yake ya “Zaidi ya Mama” ili kuwatuza waandishi wa habari na wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari katika eneo la Afrika Mashariki ambao watakuwa wamefanya vizuri katika kuandika habari zinazoelewesha, kuelimisha na kuhabarisha ambazo zitaweza kujenga jukwaa la majadiliano kuhusu ugumba ndani ya Afrika. Hafla ya kutoa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2017.
Lengo la tuzo hizo ni kujenga uelewa kuhusu mchango muhimu ambavyo vyombo vya habari vinaweza kuutoa katika kuondo unyanyapaa uliojikita katika tatizo la ugumba. Hali kadhalika zinalenga utamaduni mbovu wa kuwabagua na kuwadhalilisha wanawake na papo hapo kuuelimisha umma kuhusu kuzuia ugumba, kuisimamia hali hiyo na ugumba kwa wanaume. Nyongeza katika kampeni hiyo ni kwamba inalenga kutoa msukumo kwa wanawaume kujadili hali yao ya ugumba kwa uwazi, kuwasaidia wake zao katika safari zao za kupimwa na kutibiwa.
0 comments:
POST A COMMENT