HATIMAE AISHI MANULA AREGEA, KUUNGANA ME WENZAKE MUDA WOWOTE | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Thursday, July 27, 2017

HATIMAE AISHI MANULA AREGEA, KUUNGANA ME WENZAKE MUDA WOWOTE

Kipa Aishi Manula anatarajia kuondoka kesho kwenda Afrika Kusini kuungana na Simba.

Taarifa zinaeleza, Manula takwenda kuungana na wenzake ambao tayari wako kambini wakiendelea na mazoezi.

Awali kumekuwa na taarifa kwamba kwa kuwa mkataba wake haujaisha na Azam FC, amekuwa na hofu ya kuweka wazi kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba.

Lakini taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza, Manula anaondoka kwenda Afrika Kusini kesho.

Tayari John Bocco, Salim Mbonde ni kati ya wachezaji wapya waliotua kambini Afrika Kusini.

Kuna taarifa nyingine zinaeleza, Simba na Azam FC, wamefikia mwafaka wa siku hizo chache za mkataba zilizobaki.

Hofu ya Simba ilikuwa ni Manula kukosa mechi ya Simba Day itakayochezwa Agosti 8.


Lakini ilionekana wakifuata sheria, kwa kuwa mkataba wake unaisha baada ya muda wa usajili, angeweza kutakiwa kusajiliwa ili aichezee Simba wakati wa dirisha dogo.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT