Hivi karibuni Rais Magufuli akiwa kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa Kigoma, alimsifia na kumpongeza Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, Daivd Kafulila kwa kuliibua sakata la Tegeta Escrow ingawa wengine walimuita Tumbili.
Ayo TV na millardayo.com zinaye David Kafulila kwenye EXCLUSIVE interview na moja ya mambo aliyoyatolea ufafanuzi ni pamoja na namna alivyolipokea jambo hilo la kuitwa Tumbili.
“Mara ya kwanza nilizungumza wakati wa hotuba ya Waziri Mkuu, nikairudia wakati wa hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini. Nilipoirudia nikaipiga sana aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema akapanic, akaanza kunitusi akasema huyu Kafulila sio lolote ni kama Tumbili tu ambaye hawezi akasababisha chochote katika nchi hii.
“Nilitabasamu…mi naamini katika hoja, kwamba nikiweka hoja utaipangua kwa hoja. Kwa hiyo, ukitukana nakudharau tu nakuona kama umepanic na umeshindwa hoja. Nilicheka tu nikamwambia bwana wewe ni mwizi. Hapa tunazungumzia wizi na wewe ni mwizi unatakiwa ujibu hoja na si vinginevyo.” – David Kafulila
.
.
0 comments:
POST A COMMENT