Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameshuka katika nafasi ya watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51.
Jarida la Forbes limeripoti kwamba mali ya dangote imepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushushwa thamani kwa sarafu ya Nigeria.
Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa simiti, sukari, na unga wa ngano.
- Kampuni ya Dangote yaruhusiwa kuchimba mkaa Tanzania
- Dangote kuinunua Arsenal katika kipindi cha miaka 4
- Rais Magufuli akutana na Dangote
Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Hapo jana Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.
0 comments:
POST A COMMENT