MSUVA HAIWAZIA LA LIGA
Ndio hivyo tena safari ya Simon Msuva imeiva sasa kuelekea Morocco kuanza maisha yake mapya Difaa Hassani El Jadidi ya Morocco.
Msuva ataondoka Dar kesho Jumatano Julai 26, 2017 akiwa tayari ameshapata baraka zote kutoka uongozi wa Yanga pamoja na wachezaji wenzake.
Leo Julai 25, 2017 amezungumza na Sports Extra na kueleza matarajio pamoja na mipango yake baada ya kufika Morocco. Amesema anatamani kucheza La Liga (ligi kuu Hispania) hivyo Morocco ni njia kwake kuhakikisha anafikia malengo yake.
“Matarajio yangu nicheze lakini nisogee mbele zaidi kwa sababu pale ni karibu na nchi mbili za Ulaya, natamani nikacheze ligi ya La Liga,” Simon Msuva amemwambia Prisca Kishamba wa Sports Extra.
Leo Msuva amewaaga wachezaji wenzake, benchi la ufundi alipokwenda mazoezini kutoa mkono wa kwa heri.
Timu nzima ya shaffihdauda.co.tz inamtakia kila la heri Msuva huko aendako na kumuombea atimize ndoto na malengo yake aliyojiwekea.
0 comments:
POST A COMMENT