Mtanzania Emily Mgeta ameiwezesha timu yake ya VfB Eppingen kuibuka na ushindi wa kwanza akiwa anaichezea kwa mara ya kwanza katika mashindano.
Mgeta ambaye ni beki wa kushoto wa zamani wa Simba ameonyesha kiwango cha juu wakati VfB Eppingen ikiitwanga TSG Weinheim kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Ujerumani.
Mechi hiyo ni kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Ujerumani maarufu kama Germany Polka.
Mgeta alicheza kwa dakika zote 90 huku akiongoza kwa kupiga krosi nyingi langoni mwa TSG ambao mwanzoni walionekana kama watashinda mechi hiyo kabla ya mambo hayajawageukia.
Kawaida, timu za madaraja mbalimbali hucheza michuano ya awali kupata nafasi hiyo.
Mgeta ambaye amekulia kisoka mkoani Mwanza, amejiunga na timu hiyo ya VfB Eppingen msimu huu
0 comments:
POST A COMMENT