Mshambuliaji mpya wa Simba, John Bocco ametua katika kambi ya Simba nchini Afrika Kusini.
Mshambuliaji huyo mpya amejiunga na Simba akitokea jijini Dar es Salaam ambako alikaa kwa siku chache baada ya kurejea akitokea nchini Rwanda alipokwenda na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Bocco aliyekuwa nahodha wa Azam FC, kwa mara ya kwanza ataanza kuonekana na kikosi cha Simba Agosti 8.
Siku hiyo ni sherehe za Simba Day na wachezaji wote watatambulishwa kwa mashabiki na wapenda soka.
Hii ni mara ya kwanza Bocco kujiunga na timu tofauti ya Azam FC ambayo alipanda nayo daraja Ligi Kuu Bara na kuisaidia kubeba ubingwa wa Bara mara moja, Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii.
0 comments:
POST A COMMENT