Polisi wa Florida wamesema hawatowafungulia mashtaka ya kosa la mauaji wavulana watano ambao walitumia simu kumrekodi mtu mmoja aliyekuwa anazama kwenye bwawa la maji hadi kufa bila kumsaidia wala kutoa taarifa Polisi.
Katika video ya urefu wa zaidi ya dakika mbili, wavulana watano wa umri wa kati ya miaka 14 na 16 wanasikika wakicheka huku wakimrekodi kwa simu mtu mmoja aliyekuwa anazama kwenye bwawa jirani na nyumbani kwao Florida.
Licha ya mtu huyo kuomba msaada, wavulana hao waliendelea kulirekodi tukio hilo kwa simu huku wakicheka hatua za mwisho wa mhanga huyo wakisikika wakisema “Anakufa” lakini hawakwenda kutoa msaada wala hawakutoa taarifa.
Polisi wanasema tukio hilo lilitokea July 9, lakini wavulana hao licha ya kulirekodi hawakutoa taarifa kwa mamlaka hivyo kuufanya mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Jamel Dunn aliyekuwa na umri wa miaka 31 kukaa kwenye maji kwa zaidi ya siku nne hadi pale familia yake ilipotoa taarifa za kupotea kwake July 12 na mwili wake ukaopolewa kwenye maji July 14.
0 comments:
POST A COMMENT