Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kura nyingi Rwanda | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Saturday, August 5, 2017

Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kura nyingi Rwanda


Rwandan President Paul Kagame arrives to cast his vote at a polling station in Kigali, 4 AugustHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKagame alipiga kura mjini Kigali
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.
Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.
Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana
Paul Kagame, Frank Habineza and Philippe MpayimanaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na Philippe Mpayimana
Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.
Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.
Supporters of the ruling Rwandan Patriotic Front (RPF) carry a poster as they attend a campaign rally on August 4, 2010 in Kigali ahead of next week's presidential election.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPaul Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 na kura asilamia 93

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT