KILICHOMKUTA SINGANO NA KUSHINDWA NA WAMOROCCO | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Wednesday, August 2, 2017

KILICHOMKUTA SINGANO NA KUSHINDWA NA WAMOROCCO

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano, yuko njiani kurejea nchini akitokea Morocco alipokwenda kufanya majaribio katika timu ya Difaa Hassan Al Jadid inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.
Sababu kubwa iliyotajwa mpaka Singano kurejea Bongo ni kutokana na wakala wake aliyempeleka katika majaribio hayo kuonekana kwenda kinyume na makubaliano.
Mtu wa karibu na Singano, amesema: “Tatizo kubwa ambalo limemfanya arudi ni wakala wake wa kule anayeitwa Khalid ameshikwa na tamaa kwa sababu makubaliano ya hapa ilikua akifika anasaini moja kwa moja, lakini haikuwa hivyo.
“Tunashangaa baada ya kufika kule eti Ramadhan anafanya majaribio, lakini katika majaribio hayo, amecheza mechi sita na amefunga mabao mawili huku akitoa pasi mbili za mabao na mechi ya mwisho amecheza pamoja na Msuva.
“Sasa wakala baada ya kuona amefanya vizuri kwenye mechi hizo, akashikwa na tamaa, akaongeza dau na tukimuuliza hajibu meseji na wala hatoi ushirikiano, hivyo tumemwambia arudi na kama watamuhitaji basi ataenda tena. Ilifikia wakati akikutana na Ramadhan anamkimbia. Bora awahi kurudi maana usajili huku unakaribia kufungwa.”

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT