Agost 1, 2017 klabu ya Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Mnara, imethibitisha kuwa Haruna Niyonzima ni mchezaji rasmi wa klabu hiyo ikiwa ni siku moja tangu nyota huyo amalize mkataba na klabu ya Yanga.
Niyonzima alijiunga na Yanga mwaka 2011 akitokea APR na amedumu ndani ya Jangwani kwa miaka sita (6) lakini hatimaye ameachana na klabu hiyo na kuelekea upande wa pili kwa watani wa mabosi wake wa zamani.
“Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba tumeshamalizana nae, ameshamaliza mkataba na club aliyokuwa anaitumikia atakuja Simba. Anaweza akaenda South Africa kuungana na kikosi au anaweza kuja moja kwa moja Dar katika safari moja na Rayon Sport na atacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports siku ya Simba Day,” – Haji S. Manara Afisa Habari Simba SC.
Hapa chini unaweza kuangalia video wakati Manara akithibisha kwamba Niyonzima ni mchezaji wao mbele ya waandisi wa habari.
0 comments:
POST A COMMENT