Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 1, 2017 imeahirisha kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na wenzake hadi saa sita Mchana hatua iliyokuja baada ya Wema kuwa na udhuru.
Wema Sepetu alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Wakili wake ana udhuru, kwa sababu yupo Mahakama Kuu kwenye kesi nyingine ambapo hata hivyo, upande wa mashtaka umedai kwamba kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa na shahidi wake ni Mkemia Mkuu, hivyo asipokuja leo atashindwa kumpata kwa sababu anasafiri sana.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi saa sita mchana.
0 comments:
POST A COMMENT