Katika
Sherehe za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Parking
wilayani Nzega mkoani Tabora; Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe.
Hussein Mohammed Bashe amekabidhi hundi ya kiasi cha Shilingi za
Kitanzania Milioni Tatu na Laki Tisa (Tzs 3,900,000) kwa ajili ya
kuwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali vilivyojitokeza kwenye
sherehe hizo kuweza kumudu gharama za uendeshaji wa ofisi zao.
Hundi
hiyo ilikabidhiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Amour Hamad
Amour ambaye hakusita kusifia juhudi za Mheshimiwa mbunge kila mahali
alipotembelea miradi ya maendeleo na huduma za jamii iliyokuwa
anatekelezwa na Mhe. Hussein Bashe jimboni kwake na ndani ya Halmashauri
ya Mji wa Nzega.
Bw.
Amour H. Amour anasema.... "Tumetembea maeneo mengi, majimboni na
wilayani, tumezunguka tukiukimbiza Mwenge kila mahali; wabunge
wamejitokeza kushiriki zoezi hili lakini Mhe. Bashe amekua nasi bega kwa
bega na ushirikiano wake umekua ni mkubwa sana. Haitoshi mambo
anayoyafanya kwa wananchi wake ni mambo makubwa, ya kuigwa na kuungwa
mkono"
Kwa
upande waje Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula
alisema...."Kiongozi wa mbio za Mwenge, kuna msemo usemao msifie mtu
angali yupo hai; nami leo nasema Mhe. Bashe anafanya kazi kubwa sana.
Hapa tulipo tayari Mhe. Bashe amewapa ufadhili na amewalipia ada
wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha Tano kwenye shule
mbalimbali za serikali nchini, haitoshi bado anapambana kuhakikisha
elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini inakua na ufaulu unaongezeka"
Mhe.
Ngupula anaendelea...."Mhe. Bashe ametoa fedha taslimu na vifaa kwa
walimu na wanafunzi wote waliofaulu jimboni kwake. Kwangu mimi mbali na
mengine yote haya tu yaatosha kusema kuwa mbunge huyu anafanya mambo
makubwa na ya upendo sana kwa wananchi wake"
Aidha
Mhe. Bashe amekabidhi jumla ya Tzs 1,900,000 kwa ajili ya kununulia
vifaa na madawa kwa kikundi cha Fatilika Leather Shoes ambacho
kinahusika na Uchakataji wa Ngozi na utengenezaji wa viatu pamoja na
bidhaa nyingine za ngozi.
Uwekezaji
wa Mbunge katika kikundi hiki kunatokana na msukumo wake wa kuhakikisha
Nzega kunakuwa na kiwanda kikubwa cha Kuchakata Ngozi na kutengeneza
viatu; na tayari mpaka sasa kwa kushirikiana na Halmashauri
wamefanikisha kukipatia kikundi hiki eneo maalum na majengo kwa ajili ya
kuendeshea uzalishaji wa bidhaa na baadae kuwa na kiwanda cha Ngozi na
viatu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.
Ikiwa
ni mwaka mmoja na nusu wa ubunge wake Mhe. Hussein Mohammed Bashe
amefanikiwa kutoa mikopo na fedha mbalimbali za uwezeshaji kwa zaidi ya
vikundi mia moja vya ujasiriamali ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.
Uwezeshaji
huu unaendana na mipango ya Mbunge katika kuhakikisha anainua maisha
ya wananchi moja kwa moja kupitia vikundi vya wajasiriamali jimboni
kwake na ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Mwaka
2016, Mheshimiwa Hussein Bashe kwa kushirikiana na Airtel Tanzania
walizindua mradi wa kutoa mikopo yenye riba nafuu ya asilimia moja.
Mradi huu ulianza kunufaisha jumla ya vikundi 20 ambavyo vilikuwa na
wajasiriamali 100 na mpaka kufikia mwezi Machi 2017 jumla ya
wajasiriamali 200 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini walikuwa tayari
wamenufaika na fedha kutoka katika mradi huu uliojulikana kama
WanaNzengo Airtel Fursa.
Lakini
yote hayo hayakutosha; Mheshimiwa Bashe aliendelea kuvisimamia na
kuvisaidia vikundi mbalimbali vya wajasiriamali jimboni kwake kwa
kuanzisha dawati maalumu linaloshughulikia masuala ya Uwezeshaji katika
Ofisi ya Mbunge iliyoko katika Mtaa wa Uzunguni, Nzega Mjini.
Dhamira
kuu inayomsukuma Mhe. Bashe ni kuona kuna mabadiliko makubwa ya
kiuchumi na hali za maisha ya wananchi wake ili kuweza kuendana na kasi
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
katika kuhakikisha nchi yetu inakua ya Viwanda na Uchumi wa Kati huku
hali ya maisha ya mtanzania mmoja mmoja ikiimarika na kupunguza
utegemezi na misaada ya bajeti kutoka nje.
Mhe.
Hussein Bashe anaamini ya kuwa "watu ni masikini sio kwa sababu
wamezaliwa masikini ila wamekosa elimu na uwezeshaji ili kuweza kubuni
na kuanza miradi na biashara ambazo zitabadili maisha yao"
0 comments:
POST A COMMENT