NDEMLA HUYOOOO ULAYA | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Monday, July 24, 2017

NDEMLA HUYOOOO ULAYA

Safari ya kiungo Said Ndemla kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC ya Sweden imewadia.

Hii ni baada ya klabu ya Simba kutoa ruhusa kwa kiungo huyo kwenda kufanya majaribio.

Mwishoni mwa msimu wa mwaka jana, Simba waligoma Ndemla kwenda kufanya majaribio AFC ya Sweden ambaye anaichezea Thomas Ulimwengu kwa kuwa walikuwa wakimhitaji.

Simba walitoa sababu kwamba walikuwa wakimhitaji Ndemla katika mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara pia Kombe la Shirikisho.

Ingawa uongozi wa Simba umekuwa hautaki kulifafanua suala hilo, taarifa za uhakika zinaeleza Ndemla ameishapata visa na anaweza kuondoka nchini wakati wowote kwenda Sweden.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT