MABINGWA WATETEZI, CAMEROON. |
Unaweza kusema Tanzania ishindwe yenyewe baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kuongeza timu nane.
BAdala
ya timu 16, sasa michuano hiyo itakuwa na timu 24, maana yake timu
zilizo katika nafasi ya pili katika makundi kuwania kufuzu zitapata
nafasi ya kucheza.
Hii
inaanza moja kwa moja katika michuano ya mwakani yaani 2019
itakayofanyika nchini Cameroon ambao ndiyo mabingwa watetezi wa michuano
hiyo.
Hii ni nafasi ya Taifa Stars kuingia kwenye Afcon kwa mara nyingine tena tokea mwaka 1980.
Mara kadhaa, Taifa Stars imekuwa ikifanikiwa kushika nafasi ya pili na si ya kwanza.
Huenda kama juhudi zitafanyika, maana yake Taifa Stars ina nafasi kubwa ya kushiriki kama itajipanga sahihi
0 comments:
POST A COMMENT