Klabu ya Yanga kupitia mmwenyekiti wa Usajili imethibitisha kwamba bado hawajamaliza zoezi la usajili wa ndani na akisisitiza bado kuna bomu lingine linakuja kutoka Dar es Salaam.
Inasemekana bomu hilo ni kutoka Azam Fc ambapo uongozi wa Yanga upo mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Timu ya Taifa na Klabu ya Azam Himid Mao Mkami ambae mkataba wake na Azam Fc unaelekea ukingoni.
Yanga wanataka kuimarisha safu yao ya eneo la kiungo licha ya kumsajili Raphael Daud na Kabamba Tshishimbi lakini wanamtaka pia Himid Mao anaemudu kucheza eneo la kiungo mshambuliaji na mkabaji pia.
Taarifa za awali ambazo SokaOnline limezinasa ni kwamba Yanga watafunga rasmi zoezi la Usajili tarehe 6 mwezi huu ambapo kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati yao na Singida United.