Kampuni
ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa leo imetoa shukrani kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa kutoa baraka na
kufanikisha ziara ya klabu ya Everton ya Uingereza.
Kauli
hiyo, imetolewa ikiwa ni siku chache tangu mechi ya kirafiki kati ya
Gor Mahia na Everton ichezwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Katika mchezo huo, Everton iliyoongozwa na nahodha wa zamani wa Manchester United ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za kampuni hiyo, Masaki jijini Dar
es Salaam Mkurugenzi, Maendeleo na Uendeleshaji, Tarimba Abbasi alisema
serikali imesaidia mengi katika ziara hiyo.
Tarimba
alisema, wanalishukuru Jeshi la Polisi, Bodi ya Utalii Tanzania (TBB),
Uhamiaji, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo chini ya waziri wake, Harrison Mwakyembe kwa
kufanikisha ziara huyo.
“SportPesa
tuchukue nafasi hii kuzipongeza wizara mbalimbali hapa nchini
zilizoshiriki kufanikisha ziara ya Everton, kiukweli kabisa ziara hii
imeweza kuitangaza vema Tanzania.
“Pongezi
nyingi ziende rais wetu Magufuli, Mwakyembe mwenye dhamana ya michezo
bila kuzisahau taasisi mbalimbali ikiwemo bodi ya Utalii, Uhamiaji na
TFF,”alisema Tarimba.
mwisho
0 comments:
POST A COMMENT