Kesi
ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba, Rais wa
Evans Aveva na Makamu Rais, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imetajwa leo Julai
20 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Aveva
na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba
na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa
rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
Aveva
peke yake aliweza kufika mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na taarifa
za nje ya mahakama zimeeleza kwamba Kaburu akishindwa kufika mahakamani
kutokana na kudaiwa kuwa ni mgonjwa.
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande baada ya kesi yao kuahirishwa na sasa watarejeshwa mahakamani hapo Julai 31, mwaka huu.
Kabla ya kesi hiyo kutajwa wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.
Awali kulikuwa na taarifa huenda leo wangepata ahueni na kuachiwa kwa dhamana
0 comments:
POST A COMMENT