Usiku uliopita kulikuwa na mtanange mwingine wa Manchester United ambapo walikuwa uwanjani kucheza na mabingwa wa Champions League Real Madrid.
Katika mchezo huo dakika 45 za mwanzo ziliisha kwa United kuongoza kwa bao moja kwa sifuri bao ambalo lilifungwa mwishoni mwishoni mwa kipindi cha kwanza na Jesse Lingard.
Kipindi cha pili Madrid walijitahidi kusawazisha bao hilo ambapo dakika ya 69 walifanikiwa kupata penati na kiungo wao Casemiro hakufanya ajizi aliutumbukiza mpira nyavuni.
Goli la Casemiro liliufanya mchezo huo kumalizika dakika 90 kwa sare ya bao moja kwa moja na ndipo muamuzi alipoamuru ipigwe mikwaju ya penati.
Katika hatua ya matuta ndipo Real Madrid walikufa kwani United walishinda matuta 2 huku Madrid akishinda 1 katika mchezo huo ambao Anthony Martial wa United alikuwa katika kiwango cha hali ya juu mno.
Huu ni muendelezo wa vichapo vya United kwanj tangu pre season ianze wameshinda michezo yote na wiki iliyopita waliwafunga wapinzani wao wakubwa kutoka jiji moja klabu ya Manchester City.
0 comments:
POST A COMMENT