Kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas amemuonya Mhispania mwenzake Alvaro Morata kuhusu ugumu ambao anaweza kuupata akiwa na klabu ya Chelsea.
Fabregas anaona mashabiki wengi wa Chelsea kwa sasa wanamuangalia Morata kama mtu ambaye atafanya kile Diego Costa alichokuwa akikifanya akiwa na Chelsea.
“Sina mashaka naye hata kidogo ni mshambuliaji nwenye kila kitu lakini ukiwa hapa watu wanataka upambane ufunge kila siku katika mashindano yote kama alivyo Costa” alisema Fabregas.
“Hapa pia yupo katika timu kubwa na atakuwa katika presha kubwa sana ila uwepo wake na Batshuayi unaweza kusaidia kwa kuwa wanavipaji vikubwa na bado ni wadogo”
Alvaro Morata anaweza kubebeshwa majukumu makubwa Chelsea kwani kwa sasa Eden Hazard ni majeruhu,Pedro naye ameumia huku Diego Costa akiwa yuko mbioni kuondoka Chelsea.
0 comments:
POST A COMMENT