MAATAA WA SIMBA MECHI MBILI SAUZ KUONYESHA UWEZO WAO | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Sunday, July 23, 2017

MAATAA WA SIMBA MECHI MBILI SAUZ KUONYESHA UWEZO WAO

Skwadi ya Simba ambacho kimepiga kambi nchini Afrika Kusini, ndani ya wiki hii kitaanza kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.

Kikosi hicho ambacho kiliondoka nchini Jumatatu ya wiki iliyopita, kwa wiki nzima kimekuwa kikifanya mazoezi makali chini ya Kocha Mkuu Joseph Omog pamoja na msaidizi wake, Jackson Mayanja.

Simba ambayo itakuwa huko mpaka mwezi ujao, inatarajiwa kurejea nchini Agosti 6, mwaka huu kabla ya kufanyika kwa tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Agosti 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Akizungumza kutoka Afrika Kusini, Mayanja alisema baada ya kufanya mazoezi ya nguvu kwa wiki nzima, wanatarajia wiki hii kuanza kucheza mechi za kirafiki bila ya kufafanua dhidi ya timu gani.

“Wiki ijayo (wiki hii) ndiyo tunatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki, mpaka sasa bado sijafahamu ni dhidi ya timu gani tutakazocheza nazo, lakini mipango ipo hivyo.

“Kikubwa ambacho naweza kusema, mazoezi yetu yanakwenda vizuri tukiwa na wachezaji wachache ambao hawakuwa na majukumu na timu zao za taifa, lakini muda wowote kuanzia sasa tunaweza kuwapokea wale waliokuwa Taifa Stars pamoja na wachezaji wapya,” alisema Mayanja.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT