Kiungo wa Azam FC na Taifa Stars Himid Mao ‘Ninja’ anatajwa kuvivutia vilabu vingi vya Misri kutokana na uwezo mkubwa ambao anazidi kuuonesha ndani ya uwanja.
Kupitia mitandao mikubwa ya michezo Afrika (Africa Football Online) pamoja na vyanzo vingine kwa pamoja vimezungumzia namna Himid Mao anavyovivutia vilabu vya nchi za Misri na Afrika Kusini.
Vilabu vikubwa vya Afrika Kusini (Mamelodi Sundowns na Bidvest) pia vinahusishwa kutaka kumsaini nahodha huyo wa Stars anaevaa kitambaa cha unahodha kwa michuano ya ndani.
Mao anatajwa kuwa kwenye orodha ya viuongo bora wa kati Afrika katika kipindi hiki kutokana na uwezo wake katika eneo hilo kuzidi kuvivutia vilabu vya ndani na nje ya Afrika.
Ubora wa Mao umezidi kuonekana hususan anapocheza mechi za kimataifa ambapo michuano ya COSAFA 2017 ilizidi kuthibitisha kwamba habahatishi kwa kile anachokifanya.
Mei 1, 2017 Mao alienda Denmark kufanya majaribio kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo (Superliga).
Kutokana na kiwango chake kinavyozidi kuvutia kila kukicha, haitashangaza kumuona Himid Mao akienda kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania hata nje ya Afrika pia.
0 comments:
POST A COMMENT