MAN UNITED YASHINDA, LIVERPOOL YABAMIZWA | MABERYNEWSMEDIA
Breaking News
Loading...

Wednesday, August 2, 2017

MAN UNITED YASHINDA, LIVERPOOL YABAMIZWA


Hii leo kulikuwa na mitanange mitatu mikubwa lakini mechi ambayo ilikuwa ikifuatiliwa na wengi ni ile ya fainali ya Audi kati ya Liverpool zidi ya klabu ya Atletico Madrid.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya moja kwa moja katika dakika 90 lakini katika mikwaju ya penati kiungo wa Liverpool Henderson alikosa tuta muhimu huku Atletico wakishinda yote na hivyo Atletico kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.
Manchester United nao wamemaliza michezo yao ya kirafiki kwa ushindi wa bao 2 kwa 1 zidi ya Samdoria huku mabao ya United yakiwekwa kambani na Henrikh Mikhtaryan na Juan Mata na lile la Samdoria likifungwa na Dennis Praet.
Lakini kabla ya michezo hiyo kulikuwa na mtanange mwingine mkubwa ambapo Napoli waliichapa Bayern Munich mabao 2 kwa 0 mabao ya Napoli yakifungwa na Kalidou Koulibaly na Giacherrini.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT